LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2023

MWL NYAMKA: WACHUKULIENI HATUA VIONGOZI WASIO WAADILIFU

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Nyamka ameagiza hatua za kisheria kuchukuliwa kwa viongozi wote wasio waadilifu bila kujali wana nyadhifa gani.




"Kiongozi anapaswa kuwa kimbilio, hivyo anapoonekana anawaumiza wananchi anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote," alisema Mwl. Nyamka akiwa katika ziara ya kutembelea mabalozi katika kata ya Kibaha.

Mwl. Nyamka anasema CCM ni chama kilichoanzishwa kwa lengo la kusaidia jamii, sio kuwaumiza.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Clemence Kagaluki na Katibu wa UVCCM wilaya hiyo , Amina Makona
"Sijui kama wapo au hawapo, lakini kama katika mtaa au kata yoyote kuna kiongozi ambaye sio muadilifu, agizo langu ni kwamba achukuliwe hatua kama mtu mwingine yeyote," anasisitiza mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages