LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 25, 2023

MRADI WA MAJI BUTIMBA WA SH. BILIONI 69 WAFIKIA ASILIMIA 94 KUKAMILIKA

Butimba, Mwanza

Ujenzi wa mradi wa maji Butimba Jijini Mwsnza, unaotekelezwa na Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa Sh. Bilioni 69 umefikia asilimia 94, kukamilika.


Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema, kukamilika awamu ya kwanza ya mradi huo kutawezesha kuongeza upatikanaji wa maji kutoka lita milioni 90 za sasa kwa siku hadi lita milioni138, na utaanza majaribio ya kutoa maji Septemba 15 mwaka huu..


Aweso amesema mradi huo utanufaisha wakazi wa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyamazobe, Nyahingi, Buganda, Luchelele, Lwanhima, Sahwa, Fumagila, Kishiri na Igoma kwa upande wa Jiji la Mwanza.


Kwa upande wa Wilaya ya Misungwi alitaja maeneo ya Usagara, Nyashishi na Fella wakati kwa upande wa Magu ni Kisesa, Bujora na Isangijo.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages