LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 3, 2023

MACHINGA, BODABODA WAMPONGEZA RAIS SAMIA, WAUNGA MKONO ASILIMIA MIA MOJA UWEKEZAJI BANDARI

Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Wafanyabiashara Machinga na wasafirishaji wa bodaboda na Bajaji wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazozifanya za kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na wakati huohuo kuunga mkono suala ua Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.

Pongezi hizo kwa Rais Saimia na tamko wa kuunga mkono Uwekezaji Bandari, walivitamka mbele ya Mlezi wa Machnga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albrt Chalamila katika mkutano waliofanya jana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika risala walizosoma Kiongozi wa Machinga na wa wasafirishaji wa Bodaboda jijini Dar es Salaam, walisema, wanampongeza Rais Samia kwa sababu kazi kubwa aliyofanya inaonekana katika kila sekta ikiwemo Afya, Elimu, Biashara na Uchumi.

Walisema, ni katika jitihada zake za kuhakikisha nchi inapaa kiuchumi ndiyo sababu Serikali ya Rais Saamia inaingia katika uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam, na kwamba kwa kauli moja wanapongeza hatua hiyo kwa kuwa ni njema na inayolenga kuiliinua taifa kiuchumi.

"Sisis Maafisa  Usafirishaji (madereva wa bodaboda na bajaji) tunakunga mkono kwa sera ya uwekezaji nchini hususan Bandari ya Dar es Salaam, tuna imamni ongezeko la pato la taifa litakuwa kwa akasi na kufanikisha ukamilishaji wa miradi mikubwa kwa kwa wakati nchini, nasi tutanufaika kwa kuwa uchumi wa mtu mmoja mmoja utakua, hivyo Rais wetu tunakutia moyo tukisema piga kazi sisi bodaboda na bajaji tupo nyuma yako", walisema Bodaboda katika risala yao na kumuomba RC Chalamila wafikishie salam kwa Rais Samia.

Bodaboda walisema Rais Samia kwa sababu wamewatendea mambo mengi mema ambayo waliyataja kuwa ni pamoja na kuwapa punguzo la tozo ya pikipiki kutoka sh. 180,000 hadi kufikia 120,000, kuwapunguzia faini ya pikipiki kutoka 30,000 hadi 10,000 na kuwatambua kama kundi la wasafirishaji wadogo wadogo (Maafisa wasafirishaji wadogo).

Walisema pia Serikali inayoongozwa na Rais Saamia imewaondolea zuio la kuingia mjini kwa kuelekeza utaratibu mzuri wa kujsajiri katika mfumo wa data base na kuwapatia vituo vya kupaki katikati ya mjini.
 
Pia walisema wanaridhika na kumpongeza Rais Samia kwa kuwa Serikali anayoongoza imeunda tume ya  ya haki jinai ambayo wameieleza mengi na kero kwa bodaboda na bajaji na wametasikia yakiwasilishwa kwa Rais na wanatarajia yatafanyiwa kazi.

Kwa jumla bodaboda na machinga walisema wamelazimika kukutana ili kumuunga mkono Rais Samia bila kushawshiwa na yeyote kutokana na kazi kubwa na nzuri anazofanya katika kuleta maendeleo na ustawi wa nchi.

"Sisi wote ni mashahidi ujenzi wa madarasa nchi nzima katika kuboresha sekta ya elimu ncini, Elimu ambayo ni bure kuanzia shule ya msingi na sekondari, sanjari na utoaji ajira kw ya vifo vya kina mama na watotoa walimu.

Upande wa afya ujenzi wa  zahanati na hospitali katika ngazi za kata, wilaya na mikoa hadi kanda na ununuzi wa vifaa tiba na dawa, hali ambayo  imeendelea kwa kasi kupunguza vifo hasa vya kina mama na watoto, usafriri  Miundombiu ya  ya barabara, kilimo, usafiri wa anga, kuruhusu mabasi kusafiri saa 24, na kuleta ndege ya mizigo.

Kuhusu Utawala bora, walisema, "ni katika awamu hii ya sita ya Uongozi wa Rais Samia tumepata rais mpenda haki, mvumilivu hata watu pale baadhi ya watu wanapotoa lugha chafu dhidi yake".

Hata hivyo Machinda hayo wamelaani wale wote wanaothubutu kumtusi na kutamka maneno ya kumkejeli Rais Samia na kuomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu hao.

Machinga na bodaboda wakiwa kwenye mkutano wao wa kumpongeza Rais samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi, na pia kuunga mkono uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Bodaboda zikiwa zimeegeshwa na washiriki wa mkutano huo.
Bajaji zikiwa zimeegeshwa na washiriki wa mkutano huo.

Mlezi wa Machinga , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akizunumza kwenye mkutano huo.

Mkuu wa Wialaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza kwenye Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages