LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 7, 2023

KIWANDA KIPYA CHA MSD IDOFI NJOMBE KUOKOA ZAIDI SH. BIL. 33+video

Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Bohari ya Dawa (MSD), Hassan Ibrahimu akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Agosti 7, 2023, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya bohari hiyo.

Ibrahim amebainisha kuwa katika kufanikisha ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za afya nchini na kuendana na azma ya Serikali ya uanzishaji wa viwanda, MSD ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miundombinu ya kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idofi mkoani Njombe na kuanza uzalishaji ifikapo mwezi Septemba 2023.

 Amesema kuwa Kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa wa kuzalisha jozi za mipira ya mikono milioni 86,  kitatoa ajira za moja kwa moja kwa watu takribani 200.

Aidha, amesema kiwanda  kitachagiza uzalishaji wa malighafi ya mpira hapa nchini na kupunguza utegemezi kutoka nje ambapo fedha za kigeni sawa na kiasi cha Shilingi bilioni 33 ambazo hutumika kila mwaka kuagiza mipira ya mikono nje ya nchi.

Jukumu la uzalishaji litafanyika kupitia Kampuni Tanzu ya MSD iitwayo “MSD Medipharm Manufacturing Company Ltd” ili kuongeza ufanisi na kutoa fursa ya kushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji.

Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.




Meneja Maoteo wa MSD,  Michael Bajile akifafanua jabo wakati wa mkutano huo.

 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.


Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Hassan Ibrahimu pamoja na mambo mengine akielezea kuhusu maendeleo ya kiwanda hicho....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages