Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Bw. Willam Erio akieleza utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Agosti 2, 2023 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine, Erio amesema kuwa FCC ilifanya ukaguzi katika Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Bandari kavu (ICDs), ambapo asilimia 3.4 ya jumla ya makontena yaliyokaguliwa yenye thamani ya Sh. Bil. 20.8 yalikutwa na bidhaa zilizokiuka sheria ya alama za bidhaa.
Aidha, Erio amesema kuwa FCC ilipokea na kuyafanyia kazi malalamiko 58 ya watumiaji wa bidhaa na huduma yanayohusu mikataba inayoandaliwa na upande mmoja ikiwemo usalama wa bidhaa, upotoshaji katika bidhaa, huduma za kifedha na bima.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇