Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji wa Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akielezea umuhimu wa Baraza hilo katika mustakabali wa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari -MAELEZO, Zamaradi Kawawa akiongoza mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
PICHA ZOTE RICHARD MWAIKENDA
Ametaja mafanikio mengine kwa mwaka 2022/2023 kuwa ni;
# Baraza linaratibu jumla ya Mifuko 72 inayotoa mikopo ya moja kwa moja, dhamana, ruzuku na programu za uwezeshaji ambazo zilitengeneza jumla ya ajira 17,603,271 ambapo ajira kwa wanawake zilikuwa 9,248,916 (52.5%) na ajira kwa wanaume ni 8,354,355 (47.5%).
# Ongezeko la ushiriki wa Watanzania kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji*: (Local Content): Baraza linaratibu masuala ya Local Content katika sekta za kipaumbele ambazo ni mafuta na gesi, kilimo, ujenzi, viwanda, utalii na sekta mtambuka.
# Hadi kufikia mwezi Juni 2023, jumla ya ajira 145,245 zimezalishwa kwa Watanzania kupitia miradi mbalimbali ya uwekezaji ambapo wanawake ni 29,049 (20%) na wanaume 116,196 (80%).
# Jumla ya makampuni ya Kitanzania 2, 010 yamenufaika kwa kupata kazi mbalimbali katika miradi inayosimamiwa na kuratibiwa na Baraza.
# Mafanikio katika kuendeleza viwanda vidogo na kati (SANVN Viwanda Scheme)*: Lengo kubwa ni kutoa fursa kwa Watanzania kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, kupata mikopo yenye riba nafuu hususan kwa viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo.
# Hadi Juni 2023 mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.8 ilitolewa kwa miradi 65 katika mikoa 13.
# *Uendelezaji wa Vituo vya Uwezeshaji*:Nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma za kuwawezesha wananchi kiuchumi zinapatikana karibu na wananchi pia kupatikana katika sehemu moja inayotoa mikopo, mafunzo, urasimishaji wa biashara, ujuzi kwa wafanyabiashara, uongezaji thamani ya mazao, elimu ya kodi na upatikanaji wa masoko.
# Hadi Machi, 2023 jumla ya vituo vya uwezeshaji 18 vimeanzishwa katika mikoa 6 ya Shinyanga (Vituo 2), Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma (Vituo 6) na Dodoma (Vituo 7), Vituo viwili (Morogoro na Pwani) viko kwenye hatua za kuongeza huduma wezeshi na kuweza kuwa vituo vya uwezeshaji kamili.
# Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017nchini.
# Uanzishwaji wa kanzi data ya uwezeshaji*: Imeanzishwa kanzi data ya Taifa ya uwezeshaji ambayo lengo kuu ni kuwaunganisha wawekezaji na watoa huduma mbalimbali za biashara. Hadi kufikia mwezi Juni 2023 jumla ya watoa huduma 186 na Wawekezaji 17 walikuwa wamesajiliwa.
# Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi* ni majukwaa ambayo yako mikoa yote 26 nchini kwa ajili ya kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo mafunzo ya kujengewa uwezo katika shughuli zao za kujiongezea kipato.
# Kuanzisha na kuongoza kamati ya wanawake katika huduma rasmi za kifedha*: Hii imelenga kuwakwamua wanawake katika kupata mikopo kutoka benki na kuwaepusha kukopa kwenye sehemu zisizo rasmi na za kuwaumiza.
# Kuratibu haki na uwekezaji wa wanawake kiuchumi*: Kubuni miradi, kupewa mafunzo ya uwekezaji kiuchumi kwa wanawake ikiwemo kuwaunganisha na taasisi za kifedha.
Majukumu ya Baraza ni kusimamia uwezeshaji, kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇