LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 12, 2023

ALIYEWAHI KUWA MWENYEKITI WA SIMBA NA MWENYEKITI WA CCM TEMEKE MZEE CHAMSHAMA AFARIKI DUNIA

Na CCM Blog

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club na Mwenyekiti wa Chams Cha Msoibduzu (CCM) Wilaya ya Temeke Ayubu Chamshama amefariki dunia.


Taarifa iliyotolewa na mtoto wa Marehemu, Soud Ayubu Chamshama wa Chang'ombe Dar es Salaam, imesema Mzee Chamshama amefariki jana Agosti 11, 2023 akuwa India alikokuwa akitibiwa..


Soud amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe Maduka Mawili Dar es Salaam na maziko yanatarajiwa kufanyika Jumanne Agosti 15, 2023 kijijini kwao Kilole, Lushoto, Tanga.


Enzi za uhai wake Marehemu Chamshama mbali na kuwa Mwenyekiti wa Simba SC kwa muda mrefu na Mwenyekiti wa CCM Temeke, aliwahi pia kuwa  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Tea Blenders Ltd.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un

Mzee Chamshama, enzi za uhai wake.

Source: Issa Michuzi

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages