UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, umetamka kumuunga mkono kufa ba kupona Rais Samia Suluhu Hassan katika suala la Uwekezaji bandari.
Akizungumza leo katika Kikao cha Baraza uu la Kikatiba la UWT Ubungo Samina Mashauri amesema, katika kumuunga mkono Rais Samia wataanza kupita kata kwa kata kuhakikisha wananchi wanaelewa faida za uwekezaji huo wa bandari.
Baraza hilo limefanyika Sinza jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa viti maalum Mariam Kisangi, Mbunge wa Ubungo Waziri Profesa Kitila Mkumbo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba.
Tafadhali, msikilize Mwenyekiti Samina akizungumza kumuunga mkono uwekezaji Bandari. Bofya video hiyo.👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇