LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2023

TUZO ZA 'TISHA MAMA 2023' ZILIVYOACHA KISHINDO MLIMANI CITY, JANA, ZADHIHIRISHA UBORA WA MBUNGE JANET MAHAWANGA

Na Bashir Nkoromo, Mlimani City
Tisha Mama Foundation ni Taasisi ambayo ni matunda ya  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Janeth Mahawanga.

Taasisi hii ilianzishwa na Mbunge huyo mwaka mwaka 2021, kwa lengo la kuongeza chachu na kuhamasisha Wanawake na Mabinti kuelewa na kushiriki ipasavyo katika uzalishaji au ujasiriamali wa aina mbalimbali ili kuinuka kimamaisha na taifa kwa jumla.

"Kwa kutambua uwezo mkubwa  wa Wanawake tunataka kila mmoja  wetu  aitambue thamani yake  na awe imara  katika kuthubutu  kuanza na kidogo alichonacho kuninua kipato chake, lengo likiwa ni kufika mbali  kwa pamoja bila kumuacha mwingine nyuma.

Kwa kuzingatia haya Tisha Mama tunalenga kuhakikisha tunawajengea uwezo  wanawake na mabinti wa mkoa wa Dar es Salaam katika kufanikisha, Wanawake na mabinti tunaishi ndoto zetu, tusikubali kukatishwa tamaa kwamba hatuwezi, tuamini inawezekana!", anasema Mbunge Mahawanga.

Anasema Tisha Mama, itahakikisha Wanawake na mabinti liowahi kuwa na ndoto lakini zikakwama kufanikiwa  au walikutana na changamoto wajue kwamba sasa ni wakati wao wa kuamka na kuanza upya, wasiridhike na hali walizo nazo kwa  kuwa wanao uwezo mkubwa kuliko wanavyodhani.

Mbunge Mahawanga anawapa siri ya mafanikio wanawake na mabinti kuwa ni kuzingatia kutobubali kukosa ujasiri unaohitajika katika kufikia kilele cha safari ya ndoto zao, wafanye maamuzi, wawe wabunifu, wajitume, wahamasishane,  wawe na subira, wawajibike ipasavyo na wakubali kujifunza kupitia waliofanikiwa  na kupendana.

Katika kuhakikisha Tisha Mama inafikia lengo l, imejiwekea programu maalum ya kutambua mchango wa mabinti wanaofanya vema ndani ya mkoa wa dar es Salaam, katika nyanja mbalimbali kwa kuwa taasisi hiyo inaamini mama bora wa kesho huandaliwa leo.

Mbunge Mahawanga ambaye ndiye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Tisha Mama, anasema, Programu hiyo  hufanyika kila baada ya miezi minne  kwa kutoa vyeti vya pongezi kutambua mchango wao na kuwaonyesha mabinti wengine jinsi wenzao wanaweza.

Anasema Programu hiyo imezaa matunda sana kwa kuwa imesaidiaa mabinti wengi kutambulika hadi kwenye tuzo za Kitaifa na Kimataifa, kupata mikataba ya ubalozi wa kutaambulisha bidhaa au matangazo, na kutengeneza fursa ya ajira kwa mabinti, lakini pia inawakutanisha na mabinti wa ngazi mbalimbali kimaisha na kielimu, hivyo kuwawezesha kubadilishana nao mawazo kiasi ambacho kinawajengea kujiamini na kuwa kinamama bora wa baadaye kwenye taifa la Tanzania.

Katika kuwaunda Wanawake na Mabinti na hata Vijana wa kiume,  Tisha Mama haiishii kuwajenga kisaikolojia tu, bali huwajengea uwezo kuwapa elimu ya Ujasiriamali, Elimu ya fedha, Uchumi na uwekezaji, kutambua fursa na ubunifu na jinsi ya kujitambua na kujiamini.

Pia wanawake na mabinti kupitia vikundi vya ujasiriamali na huduma ndogo za kifedha huwakutanisha na wadau mbalimbli wa maendeleo wanaounga mkono juhudi za kumkomboa kiuchumi mwanamke wa Tanzania.

Hakai kadhalika huwapatia elimu ya kusimamia vizuri mfumo wa mawasiliano kati ya wawezeshaji na wawezeshwaji na kati ya uongozi na kina mama ili kwa pamoja wajue mwelekeo wao, kuwajengea uwezo wa kutambua  Dira  na vipaumbele  kwenye shughuli za uchumi na ujasiriamali.

Mbunge Mahawanga anasema, pia huwapatia elimu ya kuwaongezea chachu ya kujiamini na kuwa wabunifu kwenye uongozi, Ujasiriamali na hata kwenye ajira, kuwashirikisha Wanawake wajasiriamali kwenye mijadala ya kiuchumi,  na fursa ili kuwajengea uwezo wa kutunza mitaji kuleta matokeo chanya katika shughuli zao za ujasiriamali ili kuleta tija kwenye mikopo wezeshi ya asilimia 10 ambayo hutolewa na Halmashauri, kusudi marejesho yapatikane ili wanufaika wengine waongezeke.

Pia Tisha Mama huwaakutanisha  WanawakeWajasiriamali na taasisi za Kifedha, SIDO, NEEC,VETA na NSSF kwa lengo la kuboresha  maisha kupitia Uchumi wa Viwanada.

Kuwafungua zaidi Wanawake na Mabinti, Tisha Mama wamekuwa wakiwafungua akili wajue kwamba hata kuishi dar es Salaam nako ni fursa ya kipekee!

"Hivi unaelewa  suala la wewe (Mwanamke, Binti na Kijana) kuishi  kwako Dar es Salaam ni fursa kubwa sana kwako?" hivyo ndivyo Tisha Mama huanza kusema kuwaambia wanawake, Mabinti na Vijana na kisha kueleza kwa kina.

Katika Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, una fursa nyingi za kukufanya utishe,  ukilinganisha na mikoa mingine kwa sababu Dar es Salaam ndilo Jiji la kibiahara, ndio mkoa uliobeba sura ya Tanzania, sasa kwa nini usitishe? na kwa nini usiwe wewe?

"Basi Mimi Mbunge na mwakilishi wako nataka tushirikiane kuhakikisha Wanawake , Mabinti na Vijana, tunatumia tunatumia ipasavyo fursa zilizopo ndani ya Jiji hili, ni wakati wetu kumiliki viwanda, kampuni, ajira, biashara kuhakikisha uchumi wetu unakuwa imara sanjari na kuchangia pato la taifa huku tukishikana mikono ili kwenda pamoja  kufikia mafanikio. Lazima tutishe!", Anasema Mbunge Mahawanga.

TUZO ZA TISHA MAMA
Katika kuendelea kutirrisha azma yake ya kuwapongeza Kinamama na mabinti wajasiriamali wanaofanya vema katika nyanja mbalimbali ili kuwataia shime na pia kuwafanya wajulikane hadi kutuzwa Kitaifa na Kimataifa, Tisha Mama jana, ilifanya hafla ya 'kukata na shoka' ya kutoa tuzo za mwaka huu wa 2023 kwa vikundi vya Ujasiriamali vilivyofanya vema 2023.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni, hakika ili 'tisha', hasa kwa namna kina mama, mabinti na waalikwa wote walivyokuwa wamependeza huku kila mmoja akionekana kujawa na furaha muda wote.

Hafla hiyo, iliongezwa 'unene' kwa mgeni rasmi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abbas Mtemvu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) CCM, RC Mstaafu Dk. Ibrahim Msenga , Katibu wa UWT Dar es Salaam Sarah Mgoli, Mwenyekiti wa UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo na wengine mbalimbali wa CCM na Jumuiya zake, Ma-DAS, Wabunge na Madiwani.

Fungakazi ya kunogesha hafla hiyo alikuwa ni Mfalme wa Muziki wa Taarab, Mzee Yusuf ambaye mara tatu alipanda jukwaani na kutiririsha nyimbo zake kwa umahiri mkubwa jambo ambalo liliwafanya Kimama mama waliokuwa katika hafla hiyo kushindwa kuketi vitini na badala yake wakajimwayamwaaya ukumbini.

Tuzo zilizotolewa katika hafla hiyo ni pamoja na Mwanasiasa bora, utunzaji mazingira, Jukwaa la Uwezeshaji, na Ubunifu.

Akiendesha utoaji tuzo hilo Mkurugenzi wa Tisha Mama Mbunge Mahawanga, aliomba jamii kuwaunga mkono Wajasiriamali na wabunifu ambao wameonyesha kujitoa kwa ari ili waweze kusonga mbele zaidi.


Habari picha za kuwaga za hafla hiyo👇

TISHA MAMA AWARDS 2023 : KUISHI DAR ES SALAAM NI RURSA YAKO YA KWANZA, USICHULIE POA.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tisha Mama Foundation ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kuanza rasmi hafla ya utoaji tuzo kwa Vikundi vya Kinamama na Mabinti wajasiriamali, iliyofanyika jana, Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemu akisalimiana na Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo baada ya kuwasili, Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tisha Mama Foundation ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu (Wapili kulia) akishangilia na Viongozi meza kuu, baada ya kuwasili ukumbi kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, RC Mstaafu Dk. Ibrahim Msengi, Mweyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally Said, Katibu wa UWT Dar es Salaam Sarah Mgoli, Mkurugenzi wa Tisha Mama Foundation na Mbunge wa Viti Maalum mkoa huo Janeth Mahawanga na Mwenyekiti wa UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo (kulia)

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akitupia macho ratiba ya hafla hiyo baada ya kuketi. Kuia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa huo Mwajambu Mbwambo na Watatu kulia ni Mbunge Janeth Mahawanga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akiendelea kutupia macho ratiba ya hafla hiyo baada ya kuketi. Kuia ni Mbunge Janeth Mahawanga.
"Hiyo ndiyo ratiba ya shughuli yetu, bila shaka haitakuchosha", Mbunge Mahawanga akimweleza Mwenyekiti Mtemvu. 
Mwenyekiti Mwajabu akiteta jambo na Meya wa Temeke Abdallah Mtinika kwenye hafla hiyo.

Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo. 
Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo.

Geah Habibu ambaye pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Radio, akiongoza hafla hiyo.
 
Mwenyekiti wa Tisha Mama Foundation Mbunge Mahawanga akisalimia baada ya kutambulishwa na MC Geah

Baada ya Mbunge Mahawanga kutambulishwa ukumbi ukalipika, ikawa hekaheka kwa Kinamama kumshangilia wakicheza muziki wa hamasa.

Kina mama wakiendelea kumfurahia Mbunge Mahawanga huku baadhi wakijipiga naye picha kwa simu zao.
Kina mama wakiendelea kumfurahia Mbunge Mahawanga huku baadhi wakijipiga naye picha kwa simu zao.
"Hakika tumedamshi",
Kina mama wakisema huku wakiendelea kumfurahia Mbunge Mahawanga huku baadhi wakijipiga naye picha kwa simu zao.

Mbunge Mahawanga akizungumza kuhusu Tisha mama, huku washiriki wakimsikiliza kwa makini.

Katibu wa UWT Dar es Salaam Sarah Mgoli, akizungumza katika hafla hiyo.


Mjumbe wa NEC CCM, RC mstaafu Dk. Ibrahim Msengi akizungumza kweneye hafla hiyo. "Ukiona mtoto anafanya mambo mabkubwa kama haya, maana yake ni kwamba ulimlea malezi mazuri. nakupongeza sana mwanangu, lakini japo Tisha Mama mliianzisha zamani kidogo, lakini nakuomba ujue kuwa safari bado ni ndefu, ongeza juhudi...", akasema Dk. Msengi.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mweyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally Said, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meya wa Temeke, Mtinika akizungumza katika hafla hiyo.

Halafu ukafika muda wa Mzee Yussuf👇 'kukiwasha'

-------------------------------------------------

Kisha ukawadia muda wa kutoa tuzo👇

Mkurugenzi wa Tisha Mama Foundation, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga akiendesha utoaji tuzo, aliouendesha kwa kuonyesha 'documentary' ya kila aliyepata au kikundi kilichopata tuzo kabla ya mpokeaji kuitwa kupokea.

Mwakilishi wa Kikundi cha VICOBA cha BUTA cha Bunju Semeni Gama akikabidhiwa tuzo na Mwakilishi kutoka NIC. Kulia ni Mbunge Mahawanga akifurahia tukio hilo.
Semeni Gama akapiga magoti kumshukuru Mbunge Mahawanga, ambaye naye kwa upendo akamwinua kama alivyomuinua kiuchumi. Semeni alifika Dar es Salaam akiwa  Housegirl lakini baada ya Tisha Mama kumpatia mafunzo Vicoba aliyoainzisha na wenzake kwa mtaji kidogo imekuwa hadi kufikisha mtaji wa sh. bilioni Moja ikiwa na wanachama zaidi ya 300.
Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi ya kushajihisha wenye ulemabu Sophia Mbeyela akikabidhiwa tuzo na mwakilishi kutoka Azania Bank.
Sophia Mbeyela akipongezwa na Mkurugenzi wa Tisha Mama Mbunge Mahawanga baada ya kupokea tuzo hiyo.

Mkurugenzi wa Kituo cha kusaidia vijana kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya cha Kigamboni Pili Misana akipokea tuzo kutoka kwa mwakilishi wa Price Poa Perfume. Kulia ni Mbunge Mahawanga akishuhudia.
 
Mbunifu Faidha Hussein Bakari akipongzwa na Mkurugenzi wa Tisha Mama Mbunge Mahawanga, baada ya kukabidhiwa tunzo hiyo na mwakilishi wa T+MARK. Farida ambaye badi ni mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tisha Mama imemtunuku tuzo hiyo baada ya kutengeneza  ndege isiyo na rubani (drone) ambayo ina uwezo wa kupeleka ujumbe au dawa kutoka eneo moja kwenda lingine na pia kufanya umwagiliaji.
Mjasiriamali Rose Joseph akikabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo. Tisha Mama imentuku tuzo hiyo baada ya kusimamia kulipa mkopo wa sh. milioni 200 ambazo yeye na kikundi chake walikopa benki, lakini wenzake wakakimbia. hadi sasa ameshalipa zaidi ya milioni 100 kutokana na fedha anazopata kutokana na kuendesha miradi ikiwemo ya ujenzi.
Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika akimkabidhi tuzo Kiongozi wa Kikundi cha Liwalo cha Kinamama wa Kata ya Miburani Zaituni Twanga. Kinamama hao wametunukiwa tuzo kwa kufanya ujasiriamali wa uzoaji taka katika kata hiyo ya Miburani.

Mbunge Viti Maalum anayewakilisha Vyuo Vikuu Dk. Tea Ntala akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Kikundi cha Kina Mama wajenzi wa barabarea za ndani Wilaya ya Kinondoni Rahma Katundu.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akikabidhi Tuzo ya Kiongozi mahiri katika siasa, Amina Kibugila (72). Tisha Mama imentunuku tuzo Amina kutokana na kufanyakazi za Ukatibu wa CCM kwa kujitolea katika mtaa anakoishi wilayani Temeke, licha ya kwamba Katibu wa CCM wa kuchaguliwa yupo katika  eneo lake. Kwa mujibu wa Amina ni mwanachama wa CCM akitokea enzi za TANU.
 
Mwenyekiti Mtemvu akionyesha tunzo, baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Tisha Mama, Mbunge Mahawanga.

Mwenyekiti Mtemvu akizungumza  katika hafla hiyo kwa nafasi yake ya mgeni rasmi. " Nampongeza sana Mbunge Mahawanga kwa kazi hii nzuri, huu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. tungependa sana kuona Wabunge na Madiwani wa viti maalum katika mkoa huu wa Dar es Salaam wanaiga mfano huu", akasema Mwenyekiti Mtemvu.
 
Mwenyekiti Mtemvu akipongezwa na Mkurugenzi wa Tisha Mama Mbunge Mahawanga baada ya baada ya hotuba yake, Kulia ni Mwenyekiti Mwajabu Mbwambo.

Kisha hafla hiyo ikahitimishwa kwa Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mbunge Mahawanga kupigwa picha na makundi mbalimbali.👇

Mwisho kabisa Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo wakampongeza Mbunge Mahawanga👇
ENDS!

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages