Na Bashir Nkoromo, Offiacial CCM Blog
Hospital Ya Royal Polyclinic iliyopo Mnazi mmoja, karibu na taa za kuongozea magari eneo Mnazi Mmoja, imetoa ofa kwa wakazi wa Dar es Salaam, kuonana bure na Madaktari bingwa Julai 16, 2023
Taarifa ya Uongozi wa Hospitali hiyo, iliyotumwa kwetu (Blog ya Taifa ya CCM - Official CCM Blog, imewataja Madaktari Bingwa watakaokuwepo kuwa ni; Daktari bingwa wa matatizo ya uzazi na magonjwa ya wanawake(OBS/Gynacologist).
Daktari Bingwa wa watoto (Pediatrician), Daktari bingwa wa meno na kinywa (Dentist) na Daktari bingwa wa mfumo wa mkojo (Urologist).
Wengine ni Mtaalamu wa chakula na Lishe (Nutritionist), Daktari bingwa wa matatizo ya ndani ya mwili (Physician) na Daktari wa kawaida (General Practitioner)
Taarifa imesema, sanjari na kuona bure madaktari hao pia, itakuwepo nafasi ya kufanya vipimo kama vya Sukari, Presha, Joto, Uzito, Urefu, BMI na Tezi dume.
"Vipimo hivyo vyote ni bure. Hii ni katika kuisaidia Jamii ya Watanzania kwenye sekta ya Afya", imesema taarifa hiyo na kuongeza;
"Pamoja na hayo, Pia utapata nafasi ya Kuchangia Damu kupitia Shirika la Damu la Taifa ambao tutakuwa nao siku hiyo".
Taarifa imesema huduma zitaanza kuanzia muda wa asubuhi hadi saa 9 Alasiri na kwamba atakayehitaji maelezo zaidi wanaweza kuwasiliana kupitia simu 0653 663 333 au 0777 663 333 au kwa kufuatilia taarifa kupitia kurasa za Kijamii za Instagram/ @royalpolyclinicdar.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akizindua Hospitali ya Royal Polyclinic eneo la Mnazi Mmoja Jijini, siku ya Jumamosi, Julai 09, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Ahmed Suleiman. (Picha kutoka Makmataba yetu).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇