LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 18, 2023

RC MWASSA AREJEA KUTOKA KUHIJI MAKKAH

 


 

Na Lydia Lugakila,

BUKOBA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Fatma Mwassa amewasili Mkoani Kagera baada ya kukamilisha nguzo tano za uislam alipokwenda Hija katika mji wa Makkah Nchini Saudi Arabia huku akiwabebea Wana Kagera na Watanzania zawadi ya Dua pamoja na maono yenye kuwafanya kuamini kuwa tayari wamesamehewa makosa yao kupitia maombi aliyoyafanya katika ibada hiyo.


Akizungumza baada ya mapokezi yaliyofanyika katika Uwanja wa ndege Manispaa ya Bukoba  Fatma Mwassa alisema kuwa anayekwenda kuhiji akifanya hija ya kweli na kurudi salama lazima pawepo na mabadiliko ikiwa ni pamoja na mfumo wa maisha yake, kuongeza nguvu katika kumcha Mungu, unyenyekevu na hofu ya Mungu.


" Nawashukuru nyinyi mliokuja kunipokea namshukuru Mwenyezi Mungu hakika nimeongeza imani na wote waliofanikiwa kusimama Arafa Wamesamehewa ndo maana nimekuja na zawadi ya Dua" alisema Rc Mwassa.


Aidha aliyataja mambo makuu aliyoyaweka katika ibada hiyo kwa Watanzania na WanaKagera kuwa ni pamoja na kuwepo na uongozi wenye maelewano, Roho ya ushindi na yenye kutokata tamaa, kuondokana na malalamiko, ujasili wa kuamini kushinda na kuwepo mzunguko wa fedha na kupata mali.


Alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi Mkoani humo kila mtu kwa imani yake kuendelee kumcha Mwenyezi Mungu.


Ikumbuke kuwa ibada ya Hija ni moja kati ya nguzo tano za uislam na kila muumini wa dini hiyo mwenye uwezo anatakiwa kufanya safari ya siku 5 ya Hajj angalau mara moja maishani mwake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages