LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2023

NAKALA YA KITABU KIPYA KUHUSU HAYATI DK. MAGUFULI YAUZWA SH. MILIONI 1.4 MALAWI

Lilongwe - Malawi.

Nakala ya Kwanza ya Kitabu Kipya Cha Hayati  Rais Magufuli Kama kilivyoandikwa na Profesa wa Chuo kikuu Cha Hebron Nchini Malawi Prof Malango Chinthenga kimeuzwa kwa USD 600 sawa na Tsh 1,450,000/= kwa Mwananchi wa Kawaida wa Malawi ambaye alijitokeza katika Uzinduzi wa Kitabu hicho jijini Lilongwe, Kitabu hicho chenye  kurasa  461 na Chapter zipatazo 48 kimeanza kuwa Gumzo Kubwa Barani Afrika


Kitabu kinaitwa "AFRICA MAGUFULI AND CHANGE" an integrated Approach in abolishing Africa's modern economic Slavery",


kwa tafisiri isiyo Rasmi Ni "AFRIKA MAGUFULI NA MABADILIKO" Namna, Njia ya Kutokomeza Utumwa wa Kisasa wa Afrika Kiuchumi"


Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kitabu Hicho jijini Lilongwe Dr Grace Kumchulesi ambaye Ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Maendeleo ya Serikali ya Malawi anasema:


"Kutokea Hapa Malawi tutajitahidi kusambaza Kitabu Hiki katika Vyuo vyetu Vyote kwa ajili ya Vijana wetu Kujifunza Nini Maana ya Uongozi na Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka katika Ukoloni wa Kiuchumi".





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages