Na Stephano Mango, Songea.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mary Chatanda kesho Ijumaa, Julai 7, atafanya ziara katika Wilaya ya Songea Mjini mkoani Ruvuma, kukagua Utekelezaji wa Ilani na uhai wa Chama na Jumuiya zake.
Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego amesema Ofisini kwake leo, kuwa katika ziara hiyo Mwenyekiti Chatanda atakuwa pia na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa na itakuwa ziara ya siku moja.
Mgego amesema, katika ziara hiyo Mwenyekiti Chatanda atakagua miradi inayotekelezwa na Chama na miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya elimu, uchumi na miundombinu
Alisema kuwa akiwa Wilayani humo Mwenyekiti Chatanda atapata fursa ya kufanya vikao vya ndani na viongozi wa mashina, matawi na Kata, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Lizaboni
Mgego amewaomba viongozi na wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki mgeni huyo na kuhudhuria kwenye mikutano ya hadhara itakayohutubiwa na Mwenyekiti huyo na viongozi wa ngazi ya juu ya Jumuiya hiyo ya UWT Taifa
Amesema kwa namna ya pekee kabisa CCM Wilaya ya Songea Mjini inampongeza Rais Dk. Samia kwa anavyopambana kuhakikisha huduma za kiuchumi na kijamii zinawafikia wananchi, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu na usafirishaji.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Songea Mjini Veneranda Nkwera amesema maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti Chatanda kwenye Kata zote ambazo amepangiwa kwenda yamekamilika na kwamba Wanawake na Wajasiriamali mbalimbali wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kusikiliza ujumbe aliokuja nao
Nkwera amesema, Vikundi mbalimbali vya wajasiliamali na vya burudani kutoka pande mbalimbali za Songea Mjini vitakuwepo kwenye shamra shamra za mapokezi hayo.
Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda.Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego
RATIBA 👇YA ZIARA YA MARY CHATANDA SONGEA MJINI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇