Mke wa mbunge wa Lupa (Chunya), Bi Veronica Masache Kasaka akishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya DIDO Mwanafunzi Initiative Leo tarehe 12/07/2023 wameshiri katika kugawa Sare za Shule kwa watoto wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Kibaoni pamoja na Taulo za kike kwa mabinti wenye umri husika.
zoezi hili limefanyika pia katika Shule ya Sekondari Itewe pamoja na Secondari ya Makala.
akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi Mke wa Mbunge amewajuza walimu na wanafunzi kuwa kupitia ofisi ya Mbunge jimbo la Lupa (Chunya) Wataendelea kutafuta na kuziomba Taasisi zingine ili kusaidia kuwafikia wanafunzi wengi zaidi katika shule nyingine zilizopo Wilayani Chunya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇