LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2023

MIAKA 60 YA JKT YAZIDI KUNOGA, YAWAKUMBUKA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA CHAMWINO


 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) liimetoa msaada kwa akina mama waliojifungua na kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Afya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ikiwa ni  moj ya shamrashamra ya wiki ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake 1963. 

Akizungumza mara baada ya kutoa msaada wa sabuni na pampasi kwa watoto waliozaliwa ,Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa jeshi hilo,  Kanali Regina Matina amesema,katika mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Jeshi hilo  kuelekea miaka 60 ya JKT, limeona ni jambo la msingi kufanya shughuli hizo kwani nao ni sehemu ya jamii

“Huu ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali tunazozifanya  kuelekea miaka 60 ya JKT ,na hapa tumeona ni jambo la msingi kutembelea hospitalini hapa kufanya usafi na kutoa zawadi katika wodi ya wazazi kwani JKT ni sehemu ya jamii ,

“Lakini pia tumeungana na wazazi kama ilivyo majukumu ya JKT ni malezi ya vijana ,uzalishaji mali na ulinzi,na hawa ndiyo wazazi wanaotupatia vijana ,tukaona ni muhimu tusimalize maadhimisho haya bila kuwaona wazazi.”amesema Kanali Matina.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Halmashauri ya wilaya ya Chamwino John Daniel amelishukuru Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuona kituo hicho cha afya kuwa sehemu ya maadhimisho yao ya miaka 60.

“JKT tumekuwa tukishirikiana nao mara nyingi,tumekuwa tukiwaomba msaada mbaimbali na wanatusaidia ,tunaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii.”amesema Daniel

Kwa upande wake Arafa Kombe mmoja wa akina mama waliopata zawadi kwa ajili ya watoto wao amelishukuru JKT kwa zawadi hizo na kuliasa liendelee kuwakumbuka wamama huku akilitakia kila la kheri Jeshi hilo katika majukumu yake hususan ya ulinzi wa wa nchi.
















No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages