Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Toufiq amewajia juu watu wasioitakia mema nchi na kutumia suala la uwekezaji wa Bandari kujipatia umaarufu.
Toufiq ametoa kalipio hilo hivikaribuni wakati wa kikao Cha Baraza la Wanawake Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma.
"Wanawake wenzangu na viongozi naomba tusiwafumbie macho watu hao, tutambue kuwa hizo propaganda chafu zinazoendelea zina nia ovu na chafu na kusababisha mtafaruku katika Nchi yetu," amesema Toufiq na kuongeza kuwa...
"Nataka niwaambie tunaona Rais wetu ana dhamira ya dhati kabisa kutaka Tanzania ipate maendeleo, tunaona anavyohangaika huku na kule kwa ajili hiyo lakini kuna watu wasiopenda maendeleo wanaeneza propaganda za uongo."
"Suala la DP WORLD inabidi sisi tupate ufahamu sahihi na kuieleza jamii ukweli, isiwe kama propaganda zinavyoenezwa, ila yale yalikuwa ni makubaliano ya awali ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam," amesisitiza Toufiq.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇