Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena akikabidhi msaada wa vyakula kwa watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Kulelea Watoto ya Rais Samia Suluhu Hassan Kikombo jijini Dodoma Julai 5, 2023, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya Wiki ya Maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo lililoanzishwa 1963. Aliyevaa kaunda suti ni Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Tullo Masanja.
Vyakula vilivyotolewa ni; mchele kilo 500, mahindi kilo 500, maharage kilo 200, sukari kilo 50, mafuta ya alizeti, juisi, chumvi na mbuzi wawili. Sehemu kubwa ya vyakula hivyo huzalishwa na jeshi hilo.
Juzi Julai 4, 2023 jeshi hilo lilitembelea Kituo cha Afya cha Chamwino na kutoa msaada wa pampasi na sabuni kwa akina mama waliojifungua pamoja na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kituo hicho.
Aidha, jeshi hilo limeandaa maonesho ya kuadhimisha miaka 60 ya jeshi hilo yanayoendelea kwenye viwanja vya Jengo la Suma JKT jijini Dodoma. Lilifunguliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ambapo Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo Julai 10, 2023 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma anatarajiwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais Samia Suluhu Hassan.
Brigedia Jenerali Hassan Mabena akikabidhi mbuzi kwa ajili kitoweo katika makao hayo.
Askari wa JKT wakishusha kwenye lori vyakula hivyo.
Brigedia Jenerali Hassan Mabena akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo makao hayo. Wengine ni baadhi ya viongozi wa jeshi hilo, askari, watumishi wa kituo hicho pamoja na Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Tullo Masanja.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇