Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Mabibo
Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, Helen Msofe, amewataka Viongozi katika Kata ya Mabibo kufanyakazi kwa bidii, upendo na mshikamano ili Jumuiya hiyo katika Kata yao ipae na kuwa ya mfano wa kuigwa na Jumiya zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Helen ameyasema hayo, jana, wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mabibo, alipofika kujitambulisha kwao baada ya kuteuliwa hivi karibuni kuwa Mlezi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ubungo.
Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya CCM Tawi la Kanuni, Kata ya Mabibo, Helen ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ubungo, amesisitiza kuwa ili kufikia lengo la kuipaisha Jumuiya katika Kata yao ni lazima vingozi hao kuhakikisha wanakuwa wepesi kuhudhuria vikao kila vinapoitishwa.
Amesisitiza kuhudhuria vikao ni muhimu kwa sababu kiongozi asiyekuwa mwepesi kufanya hivyo atakuwa chanzo cha kudhoofisha Jumuiya katika Kata hiyo, kwa kuwa mchango wa mawazo yake utakuwa haupatikani hasa wakati huu ambao CCM inaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu 2025.
"Ndugu viongozi, mimi kwa nafasi yangu ya Mlezi wa Jumuiya yetu Wilaya ya Ubungo, nitahakikisha Jumuiya yetu katika Kata hii ya Mabibo, inapaa na kuwa ya mfano kwa jumuiya zingine, sasa ili tufike huko ni lazima kila kiongozi kuhakikisha anafanyakazi kwa bidii, upendo na mshikamano, lakini pia ahakikishe anakuwa mwepesi kuhudhuria vikao vinapoitishwa.
Tazama, kama leo, wajumbe ambao walipaswa kuwa kwenye kikao hiki hawapo, sasa hali kama hii ya viongozi kutohudhuria vikao ni hatari kwa Jumuiya, kwa hiyo nasema sijapendezwa, lazima tabia hii iachwe mara moja, mimi ni mdogo kiumri nikilinganisha na ninyi, lakini kwa kweli nitakuwa mkali, hatuwezi kwenda kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu tukiwa hivi", akasema Helen.
Katika kuonyesha nia yake ya kuiinua Jumuiya katika kata hiyo, Helen alichangia papo hapo fedha taslim sh. 100,000 (Lakini moja) kwa ajili ya mradi wa ujenzi unatarajiwa kutekelezwa na Jumuia hiyo Kata ya Mabibo, na pia kufanyia kazi suala la elimu katika Kata hiyo.
Mapema, wakizungumzia suala la kufika wajumbe wachache, Viongozi wa Jumuiya hiyo walisema kwa nyakati tofauti kwenye kikao hicho kwamba baadhi ya wajumbe wameshindwa kufika kutokana na kua katika mikimiki ya maandalizi ya Watoto kufungua shule kesho Jumatatu.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya Ubungo ambaye pia ni Mlezi wa Jumuiya Wilaya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Helen Msofe, akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mabibo, akiwa katika ziara ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa kuwa Mlezi wa Jumuiya hiyo ya Wazazi Wilaya ya Ubungo hivi karibuni. Kikao hicho kilifanyika Ofisi ya CCM Tawi la Kanuni Kata ya Mabibo, jana.Helen akisaini Kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kanuni, Kata ya Mabibo, jana.
Helen akiendelea kusaini Kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kanuni, Kata ya Mabibo, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazi Kata ya Mabibo Seif Nyuki na Katibu Tatu Baruti wakishuhudia.Helen (kushoto) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mabibo katika Ofisi ya CCM tawi la Kanuni katika Kata hiyo, kabla ya kuzunguza na wajumbe wa Baraza la Utekelezaji la Jumuiya hiyo, jana.
Helen akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazi Kata ya Mabibo Seif Nyuki na Katibu Tatu Baruti, kabla ya kuanza Kikao chake na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji.Helen akiteta jambo la Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Goba Hamis Mohamed, wakati wa Kikao chake na Baraza la Utekelezaji. Hamisi pia Ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ubungo.
Katibu wa Elimu na Malezi (EMA) wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mabibo Neema Mwinyimvua (kushoto), akizungumza wakati wa Kikao hicho.
Hilda akinukuu kwa makini badhi ya mambo aliyokuwa akiambiwa na viongozi wakati wa kikao hicho.
Katibu Tatu akizungumza wakati wa Kikao hicho.
Hilda akisikiliza kwa makini wakati mmoja wa viongozi akizungumza wakati wa Kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabibo Naffi Kinyogori akizungumza wakati wa Kikao hicho.
Hamis Mohamed akizungumza wakati wa kikao hicho.
Katibu wa EMA akizoma risala.
Mwenyekiti wa Wazazi Mabibo akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi.
Wajumbe wakiwa kwenye Kikao hicho.
Heleni akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi baada ya kikao hicho.
Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blog) inampongeza Cde Hilda kwa kikao hicho muhimu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇