Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu amesalimia Maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Kinondoni viwanja vya Tanganyika Packers.
Mkutano huo umehudhuriwa na mikoa jirani ya Pwani na Morogoro, ambapo Ndg. Gavu amewataka Watanzania kufahamu ili maendeleo yafanyike ni wajibu kwa serikali kutengeneza mfumo na kutanua wigo wa kuona inashirikiana na kuhimiza mshikamano huo katika sekta binafsi.
Aidha Gavu amesema Chama Cha Mapinduzi kitasimamia serikali katika kutekeleza Ilani ya CCM iliyoahidiwa 2020 - 2025 ili kurahisisha maisha ya kila mtanzania kwa kuzingatia ukurasa wa 18 kifungu Cha 22 Katika Ilani ya CCM.
#Kaziiendelee
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇