Wilaya ya Same ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 1.86 kimetolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu ujenzi wa vyumba 52 vya Madarasa, matundu 40 vya vyoo, Majengo mawili ya Utawala na Nyumba moja ya walimu.
Mkuu wa wilaya hiyo Kasilda Mgeni aliyeongoza kamati ya Usalama na wataalam kutoka halmashauri kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambapo amesema tofauti na maeneo mengine katika wilaya ya Same fedha hizo walipata kwa kuchelewa, hatahivyo mpango ni kukamilisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.
“Nimesisitize uadilifu hasa kwenye matumizi ya fedha lazima yaendane na kiwango cha ubora unaohitajika pia utunzaji wa Nyaraka zote muhimu za manunuzi na mchakato mzima kwenye ujenzi kuepuka kasoro zinazo weza kuibua hoja kwenye ukaguzi”Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Amemshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi huo kutoa kiasi hicho cha fedha, na kuahidi kusimamia kwa karibu kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika wilaya ya Same inakamilika kwa wakati na katika ubora unaohitajika.
“Lazima tufanye kila kinachowezekana ikiwemo kuongeza mafundi na kujenga usiku na mchana, lakini uharaka huo haimaanishi kujenga chini ya kiwango tunafuatilia kwa karibu kuhakikisha ubora wa miradi hii”.Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇