Na Mwandishi Wetu.
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk. Batilda Burian amekutana na kufanya mazungumzo na Baba Askofu Mhashamu Protase Rugambwa ambaye jana Julai 9, alliteuliwa na Baba Mtakatifu Fransisco kuwa Kardinali.
Akizungumza jana, Balozi Batilda alisema Leo Julai 10,2023 kwa niaba ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwa na wajumbe wa kamati ya Usalama tumefika Ofisini kwa Baba Askofu Mhashamu Protase Rugambwa ambaye Julai 9, alliteuliwa kuwa kardinali.
Alisema pamoja na mambo mengine, amefikisha salamu za pongezi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi huo.
"Kama viongozi wa Serikali tumemuahidi Mhashamu Baba Askofu kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha anatekeleza majukumu yake." Alisema
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇