Watu 18 abiria waliokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Same na tayari Sita kati yao wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa KCMC kwa matibabu zaidi chanzo kikielezwa ni uzembe wa Dereva ambae bado hajulikani alipo.
Aliyekuwa daktari zamu aliye wapokea majeruhi hao Dkt.Alfred Seti amesema walipokea Jumla ya Majeruhi 16 waliotokana na ajali hiyo na baada ya matibabu ya Awali wamelazimika kuwahamisha Hospitali ya Rufaa. KCMC Majeruhi Sita ambao wanahitaji matibabu ya zaidi na 10 wanaendelea kupata huduma.
Ajali hiyo imehusisha Toyota Coster yenye namba za Usajiri T819 DVD chanzo kinaelezwa NI uzembe wa Dereva kutozingatia sheria na alama za barabara ambae hata hivyo bado hajulikani alipo alitokomea kusikojulikana muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni aliefika kuwajulia hali Majeruhi hao, pamoja na kuwataka Madereva kuogeza umakini hasa wanapofika eneo la wilaya hiyo, abiria nao kuwa na tahadhari kutoa taarifa kufichua Madereva wanaokiuka sheria, kuepusha madhara kama hayo.
Wakizungumza kwa shida baadhi ya majeruhi hao wamesema chanzo ni uzembe wa Dereva kutokuwa makini hata kabla ya ajali kukaidi alama za barabarani.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Same, watu 18 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, wawili wanaendelea na matibabu kituo cha afya Hedaru, 16 walifikishwa Hopitali ya wilaya kati yao sita wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa KCMC Na 10 bado wanaendelea na matibabu Hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇