KATIBU Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo Leo anatinga Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 8 katika Mkoa wa Dodoma.
Akiwa jimboni humo, Komredi Chongolo atashiriki kikao Cha Shina namba 8 eneo la Kingiti, kukagua mradi wa Zahanati, Nyumba ya mganga na vyumba vinne vya nadarasa Shule ya Sekondari Kibakwe iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Shughuli nyingine atakazozifanya katika Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora ni; ukaguzi wa Chuo Cha VETA, mradi wa maji na josho eneo la Pwaga.
Pia, Komredi Chongolo atakagua jengo la Mama/Mtoto na maabara ya Kituo Cha Afya Rudi, atakagua barabara ya lami Kibakwe na kufanya mkutano na wananchi. Baadaye atarejea Mpwapwa Mjini kufanya kikao cha ndani na Kamati ya siasa ya wilaya.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kakagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya nwaka 2020-2925, kuhamasisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya Shina na kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇