Na Lydia Lugakila, Bukoba.
Aliyekuwa Mke wa mwenyekiti Conchesta Gervase nyomo mkazi wa mtaa wa Omukituli kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amekutwa ameuawa nje ya nyumba ya mume wake huku chanzo cha kifo hicho kikiwa hakijajulikana
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima akizungumzia tukio hilo leo Juni 13,2023 amesema, amefika katika eneo la tukio na kuongea na mkiti wa mtaa wa Omukituli Gervase Nyomo ambaye pia anafanya biashara ya kuendesha pikipiki (boda boda) amesema kuwa mwenyekiti huyo akiwa nyumbani kwake asubuhi ameitwa na mama mwenye pikipiki kuwa yuko ndani lakini nje kuna mtu amekutwa amekufa.
Amesema baada ya mwenyekiti huyo kupata taarifa za mauaji ya mtu huyo ndipo amekwenda nje kwenye tukio na kukuta mtu aliyefariki ni mke wake.
" Wakati nikiongea na mwenyekiti ambaye ni mume wa marehemu amesema asubuhi akiwa amelala aliitwa na mama ambaye ni mmiliki wa pikipiki anayoiendesha kwa ajili ya kumpatia fedha yake alipofungua aliulizwa mbona amelala wakati kwenye mazingira yake kuna tukio la mauaji, alipokwenda kushuhudia amekuta ni mke wake"Amesema Sima
Ameongeza kuwa, marehemu huyo alikuwa na majukumu ambayo yalikuwa yanasababisha kuingia ndani usiku huku mme wa marehemu alikuwa akifanya shughuli za bodaboda ambazo pia zilikuwa zinasababisha achelewe kurudi nyumbani kwake kutokana na majukumu yake.
Kwa upande wa mama mkwe wa marehemu Anajoyce Joseph mkazi wa Kibeta amesema kuwa, asubuhi akiwa anakwenda kwenye majukumu yake ameona watu wanaonyeshana akiwemo mwenyekiti ambaye ni mwanaye hakuweza kufuatilia zaidi alijua ni majukumu ya kikazi.
Ameongeza ndani ya muda mfupi amesikia sauti ya kijana wake mme wa marehemu akipiga kelele ndipo amefika aneo la tukio na kuona shingo la marehemu likiwa limejeruhiwa na kitu chenye ncha kali huku mkononi akiwa ameshika simu.
Naye shuhuda wa tukio hilo Felix France amesema kuwa, marehemu alikuwa anaishi na watu vizuri hakuwa na migogoro na majirani.
Diwani wa kata ya Kibeta Anastela Alphonce ameomba vyombo vya ulinzi na usalama kufanya shughuli yake na kuwabaini waujji waliosababisha kifo cha mwanamke huyo.
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Kagera Maketi Msengi amesema tukio analijua lipo lakini alikuwa hajalipata kwa undani
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇