Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amesema kuwa kutokana na maboresho yatakayofanywa na Kampuni ya DP ya Dubai katika Bandari ya Dar es Salaam, serikali itakuwa inapata mapato zaidi ya sh. trilioni 26 kwa mwaka ambazo ni aslimia 62 ya Bajeti ya Serikali. Ameyasema hayo mbele ya vyombo vya habari kwenye viwanja Bunge jijini Dodoma Juni 10, 2023 mara baada ya Bunge kuridhia mapendekezo ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuiendesha Bandari ya Dar es Salaam. Hivi sasa mapato yanayotokana na bandari hiyo yanafikia sh. trilioni 7 kwa Mwaka.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇