NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MAAFISA
Habari na Mawasiliano kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Hassan Khatib Hassan wametembelea
Ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujifunza shughuli zinazotekelezwa na Mfuko huo.
Akiwakaribisha
kwenye ofisi za Mfuko, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alisema Mfuko
umefurahi kutembelewa na Maafisa hao na ujio wao ni muendelezo wa ziara kama
hizo zilizowahi kufanywa na viongozi na baadhi ya taasisi za Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
“Nakumbuka
wakati mnajiandaa kuwa na chombo kama hiki, tulipokea ujumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Sheria Ndogo Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Waziri
anayeshughulikia masuala ya Kazi, Katibu Mkuu lakini pia Maafisa wa Shirika la
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), hivyo kwa kutambua uzito huo huo mtakutana na
wataalamu wetu ili wawapitishe muone jinsi tunavyotekeleza shughuli zetu.”
Alisema Dkt. Mduma.
Akifafanua
zaidi Mkuurgenzi wa Hudma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema WCF
ina Dira (vision) ya kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma ya fidia kwa
wafanyakazi barani Afrika.
“Vielelezo
vinavyoonyesha maono haya tunayatekeleza ni jinsi ambavyo mataifa mengi
yamekuwa yakipata sifa za utendaji bora wa Mfuko kupitia Shirika la Kazi
Duniani (ILO), na hivyo kuvutiwa kuja kwetu kujifunza na tayari tumepokea ugeni
kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kuisni Botswana na tumepokea maombi ya mataifa
mengine ya Ethiopia na Eswatini wote wakitaka kuja kujifunza kutoka kwetu.”
Alifafanua Dkt. Omar.
Kwa
upande wake, Mkurugewnzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Bw. Hassan Khatib
Hassan aliushukuru Mfuko kwa kuwapokea na kuwapatia elimu ambayo imewafungua ya
fidia kwa wafanyakazi
“Tuliyoyapata
ni zaidi ya yale tulioyatarajia, nichukue fursa hii kuwashukuru sana na niahidi
kwamba yote tuliojifunza tutayafanyia kazi na tutapeleka elimu hii kwa wenzetu
ili na wao wapate uelewa wa kile tulichojifunza.” Alisema Hassan.
Pamoja na kupata elimu kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015] maafisa hao pia walielimishwa kuhusu uendeshaji wa mfuko, namna ya ulipaji mafao ya fidia lakini pia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bi. Laura Kunenge aliwaeleza jinsi Mfuko unavyowasiliana na Umma kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo mikutano, semina na makongamano, machapisho, vyombo vya habari vya televisheni, redio, magazeti, na mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇