Na Richard Mwaikenda, Kongwa
KATIBU Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo, katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 8 Mkoa wa Dodoma Leo Juni 17, 2023 atatembelea iliyokuwa Kambi ya Kongwa ya Wapigania Uhuru na Ukombozi.
Akiwa katika Kambi hiyo iliyotumika kutoa mafunzo kwa wapigania Uhuru na Ukombozi wa Nchi za kusini mwa Afrika atapatiwa historia ya kambi hiyo na kupanda mti wa kumbukumbu.
Komredi Chongolo, akiwa katika Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge, Spika mstaafu Job Ndugai atakagua ujenzi wa ukumbi wa CCM, atatembelea kujua uendeshaji wa Ranchi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na kukagua uendeshaji wa Kituo Cha Afya Kibaigwa.
Aidha, atashiriki kikao cha shina namba 8 Kibaigwa, atakagua mradi wa maji Mkoka, atafanya mkutano wa wazi wa wanachama wa CCM na wananchi eneo la Songambele na kumalizia na kikao cha ndani cha Kamati ya siasa Wilaya ya Kongwa.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kakagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya nwaka 2020-2925, kuhamasisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya Shina na kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇