Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO amesema ndege kubwa aina ya Boing 767-300F ya mizigo inatarajiwa kuwasili nchini kesho Juni 3 mwaka huu na hivyo Tanzania kuandika historia kwa kumiliki kwa mara ya kwanza ndege aina hiyo.
Msema alisema hayo Jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kuanza kwa majaribio ya treni ya abiria na ndege hiyo ya mizigo.
Msigwa alizungumzia upotoshwaji uliofanywa kupitia katika mtandao wa myflyright.com ambao unatoa taarifa mbalimbali za usafiri wa anga uliochapisha taarifa za kueleza kuwa sekta ya anga Tanzania imekumbwa na kashfa nzito ya ndege yake ya mizigo aina ya Boing 767-300F kusafirisha mizigo kwa njia haramu mizigo ambayo haijakaguliwa na maafisa wa forodha na haikufuata taratibu za forodha.
Aidha, taarifa hizo zinalenga kuchafua sekta ya anga ya Tanzania na kuharibu sifa ya Shirika la ndege ATCL ambalo linaendelea kujiimarisha ili liweze kutoa huduma bora na kuchangia katika uchumi wa Tanzania.
“Nataka niwaambie kwamba taarifa hizo ni za upotoshaji na uzushi mkubwa na zipuuzwe. Serikali inaona kama taarifa hizi ni njia mojawapo ya kurudisha nyuma juhudi zake za kukuza sekta ya usafiri wa anga ni za upotoshaji kwa sababu hazina ukweli wowote”, alisisitiza Bw. Msigwa.
Aidha, alifafanua kuwa ndege hiyo ya mizigo aina ya Boing 767-300F bado haijafika Tanzania, kwa sasa iko kwa watengezezaji nchini Marekani.
Gerson Msigwa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇