Balozi na Mkuu wa Kituo cha Uwakilishi Mjini Havana, nchini Cuba Humphrey Polepole jana aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Cuba Miguel DĂaz-Canel BermĂşdez
Baada ya kuwasilisha hati Balozi Polepole alifanya mazungumzo na Rais huyo wa Cuba na pamoja na mambo mengine alimpa salamu za mshikamano kutoka kwa Samia Suluhu Hassan.
Naye, naye Rais DĂaz-Canel alimhakikishia ushirikiano mkubwa ambao umejengwa katika misingi imara na waasisi wa mataifa ya Tanzania na Cuba Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba Kamanda Fidel Castro.
Wakati uo huo Balozi Polepole alikutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Elimu ya Cuba ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya siku ya Kimataifa ya Kiswahili itakayoadhimishwa Julai 7, 2023.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇