LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 4, 2023

UJENZI BWAWA LA UMWAGILIAJI MEMBE DODOMA WAFIKIA ASILIMIA 45.83

Membe, Dodoma
Msimamizi wa mradi wa ujenzi Bwawa la Umwagiliaji lililopo Kata ya Membe Wilayani Chamwino mkoani Dodoma unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)  Mhandisi Saleh Madebe  amesema ujenzi wa Bwawa hilo umefikia asilimia 45.83.

Ameyasma hayo leo wakati Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chamwino, ikiongozwa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Sylivester Yaledi (Chief Yaledi) ilipotembelea mradi huo kukagua hatua ya utekelezaji.

Kamati hiyo imeipongeza NIRC kwa usimamizi makini wa ujenzi wa bwawa hilo litakaloweza kumwagilia zaidi ya hekari 8,000 katika mashamba ya wakulima wa eneo hilo la Membe ikiwa ni miongoni mwa miradi ya umwagiliaji inayoendelea kutekelezwa na tume.

Pamoja na kutoa pongezi hizo,  Kamati hiyo imemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili kuendana na muda wa mkataba na hatimaye mradi huo uwe na tija kwa wakulima na
kuchochea uchumi wa nchi.

Kwa mujibu wa Mkataba mradi huo unatakiwa kukamilika Septemba 1, 2023, ambapo matokeo ya kukamilika kwa mradi huo utawezesha halmashauri ya wilaya ya Chamwino na mkoa wa Dodoma kuwa na chakula cha kutosha na kuzalisha ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo. 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Sylivester Yaledi (kushoto) akimuuliza jambo Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa Maji kwa ajili ya umwagiliji  unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) Mhandisi Saleh Madebe (kulia), Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya hiyo ya Chamwino ilipotembelea Mradi huo, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages