LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 12, 2023

RAIS MSTAAFU DK. KIKWETE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU MSTAAFU WA UN BAN-KIMOON JIJINI SEOUL, KOREA KUSINI, JANA

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu (UN) Ban Ki-moon, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon jijini Seoul, Korea Kusini, jana.

Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) yuko Seoul, Korea Kusini, kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Serikali na Mashirika Mbalimbali ya Korea Kusini kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea. GPE ambayo ilianzishwa na nchi za G7 miaka 20 iliyopita, imeendelea kupigania elimu kwa ajili ya mtoto wa kike na wa kiume kwa kuomba kuungwa mkono na nchi na taasisi zinazoweza kuchangia katika elimu duniani.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages