Golden Tulip, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Waandishi wa Habari watambue kuwa hakuna uhuru usio na mipaka, wala hakuna uhuru bila wajibu hivyo kwa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kutambua uzalendo wa nchi.
Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa vyombo vya habari vinaweza kutoa mchango mkubwa endapo Waandishi wa Habari watazingatia uzalendo, weledi na maadili ya taaluma.
Amesema bila kuzingatiwa hayo ikawa kinyume chake inaweza kufifisha jitihada za maendeleo na kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika siku ya mwisho ya Kongamano la Miaka 30 ya Uhuru wa vyombo vya Habar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi
Aidha ametoa mwito kwa Waandishi wa Habari watumie fursa ya siku hiyo kuweka mkazo katika uhuru wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binadamu.
Vilevile, amewataka jumuiya na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari watumie waitumie kusherehekea na kuungana na mashirika yanayotangaza masuala ya mazingira, haki za wanawake, za watoto, za asili, za kidijitali, vita dhidi ya ufisadi na mengineyo.
Rais Dk. Mwinyi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇