Ikulu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kupitia takwimu zilizotolewa na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Serikali ina jukumu la kujipanga kwa utekelezaji wa kiuchumi na kijamii.
Ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar katika shughuli fupi ya kukabidhiwa ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanywa na Makamu mwenza wa Kamati ya ushauri wa Sensa kitaifa , Makamu pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdullah na ujumbe wake .
Matokeo ya takwimu hizo yameonesha kwamba ongezeko la idadi la Watu Zanzibar imefikia asilimia 3.7 kwa Mwaka.
Vilevile ifikapo Mwaka 2025 kuhitimisha Dira ya Maendeleo ya Tanzania, Zanzibar itakuwa na idadi ya Watu wapatao Milioni 2.08 , Dunia itakapohitimisha malengo endelevu mwaka 2030 Zanzibar inakadiriwa idadi ya watu itakuwa milioni 2.44 , na mwisho wa Dira 2050 Zanzibar inakisiwa kuwa na idadi ya watu Milioni 4.63.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇