LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 3, 2023

NDOMBA, MADIWANI KIBAHA MJINI KUTUA SHULE YA MSINGI MKOMBOZI KESHO

Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba akiwa na Makamu Mwenyekiti  Celina William (Diwani Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi).
Na Dismas LYASSA, Kibaha

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba na madiwani wa halmashauri hiyo kesho alhamisi asubuhi watafanya ziara kutembelea shule mpya ya Msingi Mkombozi (Shule shikizi ya Kidimu) azma kuu ikiwa ni kuangalia maendeleo ya shule hiyo.

Kulingana na maelezo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkombozi, Anas Bwanari, viongozi hao wanakuja kuangalia maendeleo ya shule hiyo hasa choo na d
arasa moja ambalo hivi karibuni fedha zilitolewa kwa ajili ya kuzijenga na kuboresha.

Baadhi ya wananchi wa Mkombozi wamempongeza mwenyekiti Ndomba na madiwani kutokana na kushirikiana vizuri na wananchi katika kuharakisha maendeleo.

"Wakati tunaanza kujenga hatukuamini kama tutafika hapa, lakini tunashukuru wananchi tulianza kujenga, kisha wenzetu wa halmashauri walikuja na kutusaidia kuezeka na kuongeza madarasa. Tunashukuru sana, tunaomba ikiwezekana waangalie namna ya kujenga madarasa zaidi au hata kutuongezea eneo ili ikiwezekana shule ya Sekondari ijengwe hapa hapa karibu," alisema mwananchi.

Katika mtaa wa Mkombozi pia wameanzisha ujenzi wa Zahanati ya Mtaa na iko katika hatua za kujenga msingi, wananchi wana imani kwamba halmashauri itaongeza nguvu ili kuharakisha ujenzi huo muhimu, kwani mtaa huo hauna zahanati.

Anas Bwanari, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkombozi akiwa na mwanae


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages