Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Mei 24, 2023 ameupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Pwani, katika mapokezi ambayo yamefanyika Viwanja vya Tazara, Wilayani Temeke.
Akipokea Mwenge huo RC Chalamila amesema Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam utakimbizwa katika Kilometa 499.9, ukipitia miradi 32 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 93 (93,457,467,363,.83).
Amesema miradi hiyo ipo iliyokamilika na mingine ambayi ipo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji.
RC Chalamila baabaya kupokeaMwenfe huo ameukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya Temeke ambayo ndiyo Wilaya ya kwanza kuukimbiza katika Mkoa huo.
Kwa mujibu wa RC Chalamila kesho Tarehe 25/05/2023 Mwenge huo utakabidhiwa Wilaya ya Kigamboni, Tarehe 26/05/2023 Wilaya ya Ilala, Tarehe 27/05/203 Wilaya ya Ubungo na Tarehe 28/05/2023 Wilaya ya Kinondoni na baadae utakabidhiwa Mkoa wa Kusini Magharibi, Zanzibar.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2023 unachagizwa na kauli mbiu ya "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa."
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, leo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇