Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Miradi Sita (6) muhimu ya Barabara, Maji, Elimu na Afya inatarajiwa kuzinduliwa kwa kishindo wakati mbio za Mwenge wa Uhuru zitakaporindima katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Ijumaa, Mei 26, 2023.
Taarifa iliyopatikana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo, imesema, mapokezi ya Mwenge huo yatafanyika Kituo cha mabasi ya Mwendokasi, eneo la Gerezani mtaa wa Gerezani Magharibi.
Taarifa imetaja miradi itakayozinduliwa kuwa ni Barabara eneo la Ismail Upanga katika mtaa wa Kitonga, Shule ya Sekondaro Liwiti iliyopo Mtaa wa Liwiti, Mradi wa Vijana Kitunda, Mradi ya Maji na Mradi wa Afya Zingiziwa.
Baada ya hekaheka ya uzinduzi wa miradi, Mkesha wa Mwenge utafantika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Gogo, Chanika.
Taarifa imesema katika mkesha huo kutakuwa na burudani kem kem ambazo zitakolezwa na Wasanii mbalimbali muziki wa kizazi kipya.
Wanamuziki wanaotarajiwa kuwepo katika kunigesha mkesha huo wametajwa kuwa ni Mzee wa Brax, MC Hamza, Msaagasumu, Barobaro na Kingi Manyota.
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo |



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇