LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 10, 2023

WAKAZI 26,000 KATA PANGANI KIBAHA MJINI WAMUANGUKIA RAIS SAMIA KWA KUKOSA MAJI


Ni wa mitaa nane ikiwamo Mkombozi, Kidimu, Lumumba, Pangani, Miwale na Mtakuja…hawajawahi kuwa na maji ya bomba tangu kuumbwa kwa ulimwengu

*Mradi wa maji walalamikiwa kwa kusuasua

*Wampongeza Mbunge Koka kwa kuwapambania

Na Dismas Lyassa, Kibaha

WANANCHI zaidi ya 26,000 wa Kata ya Pangani katika Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani wamemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kupata maji kwani tangu kuumbwa kwa dunia wamekuwa hawana huduma ya maji ya bomba, huku miradi ya maji inayoendeshwa katika eneo hilo ikilalamikiwa kusuasua.

“Kuna miradi kadhaa imewahi kufanyika katika kata yetu, mingine iliwahi kumalizika kabisa, lakini maji hayatoki na hatujui ni kwanini hali inakuwa hivi, tunamuomba sana kipenzi chetu, mama yetu Rais Samia aingilie kati hali mbaya ya huduma ya maji iliyoko kwenye mitaa ya kata hii  ikiwamo Mtaa wa Mkombozi, Kidimu, Lumumba, Pangani, Miwale na Mtakuja,” anasema Mama Jamila Mrema.

Wananchi wengi wanasema kutokana na ukweli kwamba Kata haina maji ya bomba, walitamani kuona miradi ya maji inatiliwa uzito utekelezaji wake.

“Tunashindwa kumlaumu Mbunge wetu  Silvestry Koka, kwa sababu mara kadhaa kama Mbunge tumekuwa tukimuona akitupigania Bungeni tupate maji, lakini watendaji wanatuangusha, hatuna maji,” anasema mwananchi mwingine Mwahamisi Haule, mkazi wa Pangani.

Jana Bungeni Mbunge Koka kwa mara nyingine aliomba tena Kata ya Pangani na mitaa yote ya Kata hiyo kupatiwa huduma ya maji.

“Jambo la maji tumelijadili sana na wizara ya maji, lakini huu ni mwaka tatu kwenda wa nne, jambo hili la maji bado halijafanyiwa kazi…wananchi wa Pangani wanasema cheche za waziri wa maji kufanya kazi bado hawajaziona,” alisema Mbunge Koka.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages