LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 14, 2023

DK.MWINYI AENDELEA NA ZIARA KUKAGUA MALI ZA CCM NA JUMUIYA ZAKE ZANZIBAR


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Zanzibar), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameendelea na ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake Zanzibar ikiwemo eneo la Amani CCM Mkoa, eneo la biashara la Wilaya Amani nyuma kwa Wazee, maeneo ya ofisi za CCM Wilaya ya Amani, miradi ya CCM ofisi ya Wilaya Mjini , kituo cha mafuta kijangwani, miradi ya maduka ya UVCCM eneo la Darajani , eneo la Afisi kuu za UVCCM Gymkhana Mkoa wa Mjini Magharibi.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake inatoa fursa ya kufuatilia na kuboresha utendaji wa mali za Chama ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuleta matokeo mazuri kwa Chama na jumuiya zake kujiendesha kiuchumi .
Kwa lengo la kuhakikisha mali za Chama zinaendeshwa na zinafaidisha Chama na jumuiya zake kwa ujumla Zanzibar.
đź—“️14 Mei 2023
đź“ŤMkoa wa Mjini Magharibi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages