ASAS ameyasema hayo wakati akizungumza na Kundi la wafanyabiara wadogo wadogo (MACHINGA) wa Manispaa ya Iringa ambao mwezi machi mwaka huu waliamishwa katikati ya Mji na kutengewa Eneo la Mlandege kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
Licha ya wamachinga hao kuhamia Eneo walio pangiwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa umeme, maji, mitaji kufa kwa baadhi ya wafanyabiara kwani wateja wengi walikuwa Bado hawajazoea Eneo jipya.
Katika kutatua hayo Asas ameutaka Uongozi wa shirikisho la MACHINGA kupeleka gharama zote hadi kufanikisha kuwekwa kwa umeme na maji katika eneo hilo pia amewaahidi kuwapatia Mtaji kwa ajili ya kunusuru biashara zao.
Ikumbukwe hii si mara ya kwanza Asas kusaidia kundi hili kwani aliwaikuwachangia Sh. Milioni 100, ambapo Sh Milioni 50 zilitumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara zao na Sh Milioni 50 nyingine kwa ajili ya mfuko wao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇