LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2023

YANGA KIDEDEA YAIBAMIZA RIVERS MBILI KWA NUNGE

 


MABAO ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kipindi cha pili yameipa Yanga ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Rivers United katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria.

Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 73, ingawa ilibidi refa Abongile Tom wa Afrika Kusini akajiridhishe kwenye VAR na la pili dakika ya 81 mara zote akimalizia pasi ya beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto.

Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katĂ­ ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages