Na CCM Blog, Dar es Salaam
Kampuni ya Ndege ya Kenya(KQ) inakusudia kuingia makubaliano na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa lengo la kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Kampuni hizo.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano kwa Umma ATCL, imesema Mtendaji Mkuu wa KQ Allan Kilavuka na ujumbe wake wamesema hayo wakati wa kikao cha awali na viongozi wa ATCL akiwemo Mtendaji Mkuu Mhandisi Ladislaus Matindi, kilichofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Ofisi za ATCL jijini Dar es Salaam.
Akifafanua, Kilavuka alisema wamelazimika kufanya hivyo kutokana na uwepo wa maeneo mengi ambayo Kampuni hizo zinaweza kushirikiana ikiwemo eneo la usafirishaji mizigo.
Alieleza kuwa Kenya ni kituo cha usafirishaji mizigo katika bara la Afrika kwa mizigo waliyonayo wanaweza kuingia makubaliano na Tanzania kuhakikisha ndege ya mizigo Boeing 767-300 yenye uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja, inatumika kikamilifu.
“Hivi karibuni Tanzania itapokea ndege yake ya mizigo ambayo itaweza kutatua changamoto ya usafirishaji mizigo kwa kiwango kikubwa, tunaamini tunaweza kushirikiana kwenye eneo hili”, alisema Kilavula.
Alisema, kwa upande wa abiria, ampuni hizoz inaweza kushirikiana katika kusafirisha abiria kwa kuzingatia misingi yenye kunufaisha pande zote mbili.
“Kupitia ndege tulizonazo, vifaa na wataalam wetu wakitumika ipasavyo tutaongeza thamani na kupunguza gharama za uendeshaji wa ATCL na KQ. Uwepo wa Boeing 787- 8 (Dreamliner) na ujio wa ndege ya mizigo Boeing 767- 300F zinafungua fursa zaidi za kibiashara", alisema Kilavula.
Naye handisi Matindi alisema kikao kimeangalia masuala yatakayosaidia ustawi wa Kampuni huzo za ndege pamoja na nchi zao kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya sokoduniani.Ametajamaeneoyanayokusudiwakushirikiananipamojanakubadilishanawataalamu, kuendeshamafunzokwavitendopasipokutegemeanchizambalinausafirishajiwamizigo, ilikuongezaufanisikatikauendeshajiwaKampunihizi.
“Soko la Afrika peke yake ni kubwa sana na linahitaji ushirikiano katika kulifikia hususani huduma ya kusafirisha abiria na mizigo. Mahitaji mengine ni pamoja na mafunzo kwa vitendo suala linalolazimu kusafirisha wataalamu kwenda nchi za Ulaya kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili au tatu. Iwapo elimu hii inaweza kupatikana nchi jirani, itakuwa bora zaidi ili kuinua uwezo wa kampuni hizo mbili na kuleta tija zaidi kwa jamii inayowazunguka” alifafanua Mhandisi Matindi.
Mhandisi Matindia metumianafasi hiyo pia kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za biashara na uwekezaji nchini baada ya ziara yake nchini Kenya,
Ziara ya Mtendaji Mkuu wa KQ imepokelewa na mwamko mpya na watendaji wa ATCL ambao wanakiri ni ishara nzuri ya kuwepo mahusiano bora ya kibiashara, kiuchumi na kidiplomasia kati ya mataifa Tanzania na Kenya hususan kwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi (kulia) akimkabidhi sampuli ya ndege Boeing 767-300F Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Kenya (KQ) Bw. Allan Kilavuka kama kumbukumbu ya mwanzo wa mazungumzo ya mashirikiano ya kibiashara baina ya ATCL na KQ baada ya kikao kilichofanyika katika ofisi za ATCL jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇