LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 18, 2023

RAIS SAMIA AMPONGEZA MWANARIADHA GABRIEL GAEY ALIYEIBUKA MSHINDI WA PILI MBIO ZA BOSTON MAREKANI

Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Gaey kwa  kushinda nafasi ya pili katika mashindano ya mbio za Boston Marathon 2023 zilizofanyika jana, Boston Massachusetts nchini Marekani.

Katika mbio hizo Gaey alitumia saa 2:06:04 kuhu nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkenya Evans Cheber aliyetumia saa 2: 2:05:54.

Rais Samia ametoa pongezi hizo jana Aprili 17, 2023 kupitia kurasa zake rasmi za mitamdao ya kijamii akisema mafanikio hayo yameipa heshima Tanzania.

"Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya riadha ya Kijamii ya Boston yaliyofanyika leo (jana) nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbela zaidi. Serikali inaendelea kuwaunga mkono wanamichezo", ameandika Rais Samia katika ukurasa wake huo wa mitandao ya Kijamii.

Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Gaey 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages