LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 1, 2023

MWENYEKITI WA CCM TANGA ARIDHISHWA UPATIKANAJI VYAKULA BEI NAFUU MGADINI NA NGAMIANI

 Na Salma Amour Tanga.

Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga kimeridhishwa na hali ya upatikanaji wa vyakula Kwa bei nafuu katika soko la mgandini na ngamiani  ambapo wafanyabiashara wengi wameweza kuelewa kuwa mwezi wa ramadhan sio mwezi wa kuwapandishia wananchi bei za bidhaa kwa  kiwango kikubwa kitakacho sababisha wengi wao kushindwa kununua vyakula.


Akizungumza na waandishi wa habari jumatano machi 29.3.  2023 Mara baada ya kutembelea masoko hao Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdul Rahman  ameeleza kuwa baadhi ya vyakula vimepungua bei  katika kipindi hiki Cha mwezi wa ramadhan ikiwa ni Moja  Mabadiliko ya uelewa juu ya wabanyabiashara hao kuwa mwezi huu  si Kwa ajili ya kuwakomoa wananchi wa kuwapandishia bei za vyakula Ili kupata fedha nyingi.


"Niwapongeze wafanyabiashara wote  wa soko la mgandini na ngamiani Kwa kuona umuhimu wa kuuzwa bidhaa zao Kwa bei za kawaida kama ilivyokuwa hapo awali,Kwa Sasa wafanyabiashara wengi wamekuwa waelewa kuwa mwezi wa ramadhan sio mwezi wa kuwakomoa wananchi Bali  mwezi huu upo Kwa Ajili ya kuchuma mambo mema"


Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kutowalaumu wafanyabiashara katika baadhi ya bei za vyakula kuwa juu Kwa kuwa wafanyabiashara hao wananunua kutoka Kwa wakulima  Ili nao wapate faida.

 .

"Wakazi wa Tanga  niwaombe kuwa na uvumilivu katika baadhi ya vyakula kama ndizi za mkono wa tembo kuwa  juu  tumeona baadhi ya wananchi wakilalamika, lakini ukweli ni kuwa mfanyabiasha anapochukua bidhaa kutoka Kwa mkulima hawezi kununua bidhaa Kwa laki akarudisha  pungufu ya hapo  lakini Zaidi ni kuwa atauza Ili  apate faida yake.


Kwa upande Wake Meya wa Tanga la Tanga Abdulrahman shiloow   alibainisha kuwa kupitia ziara hiyo fupi   ya kuangalia Hali ya bei za vyakula kwenye masoko hayo pia Kuna uhitaji wa   kuiboresha  miundombinu katika soko  la mgandini Ili kuondoa kero ya mazingira Duni  hususan katika kipindi Cha mvua.


"  Halmashauri wa  Jiji la Tanga Haina uwezo wa kujenga soko Hilo kwa sababu fedha nyingi zinahitajika ikiwa bajeti yake ni shilingi bilioni 17  na halmashauri yetu inakusanya shilingi  bilioni 18 Kwa Mwaka lakini    tumeomba Serikali kuu iweke nguvu za kutuwezesha soko Hilo kujengwa na  imetuahidi kupitia  fedha za mradi wa TACTIK kuwa itajenga soko la mgandini ambalo ndio soko kubwa lenye uhitaji Kwa wananchi wengi.


Nae pia  katibu wa soko la mgandini shabaan Mohammed shabaan imekishukuru chama Cha mapinduzi mkoani Tanga Kwa kuwajali wakazi wa Tanga hususan katika kuangalia Changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye jamii.


"Niishukuru serikali ya CCM Kwa kutujali kupitia Changamoto mbalimbali tunazokumbana nazo kwenye jamii yetu, awali  sikutarajia kuwa kama serikali yetu itawaza kufikiri  kutujengea  soko hili lakini  ninaimani soko hili likipata Mabadiliko makubwa basi wafanyabiashara wote  1,600 watauza kidhaa zao katika mazingira   mazuri na salama kabisa, ukweli ni kuwa kiafya  sio salama Kwa wanunuzi wa bidhaa za vyakula kukuta vimewekwa chini hii pia inachangia mlipuko wa magonjwa  mbalimbali Kwa walaji, na Leo nimefarijika sana kuona kuwa serikali yetu inampango madhubuti wa kutuletea maendeleo makubwa  katika mkoa wetu".


Aliongeza kuwa wafanyabiashara katika masoko mbalimbali wanajali kupata  baraka Kwa mungu wa kuzingatia sheria na taratibu za Imani ya dini ya kiislam Kwa kuwauzia wateja wao Kwa bei nafuu na sio kuwapandishia bei kama ilivyo zoeleka katika miaka ya nyuma  hususan katika kipindi Cha mwezi wa Ramadhan.


"Watu wengi wameelimika kupitia vipindi mbalimbali vya  mawaidha Kwa mashekh wetu kuwa mwezi huu mtukufu si Kwa ajili ya kutapa faida za kupitiliza  ambazo hazina Baraka,Kwa kuamini kuwa lazima wateja watakuja, Kwa hili tunawashukuru sana  watanyabiasha wote na mungu aendelee kuwabariki juu ya uadilifu wao".


Nae mfanyabiashara  wa samaki katika  soko la ngamiani  Mohamed chuo ameleza kuwa mzunguko wa biashara katika soko Hilo ni  mdogo  kitokana na kuhamishwa kwa stendi ya pangani na horohoro  kupelekwa sehemu nyingine .

*****

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdul Rahman akizungumza na wafanyabiashara katika soko ngamiani kuhusu bei mbalimbali za vyakula na Changamoto zilizopo katika biashara zao

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages