LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2023

M-NEC HAMOUD AKABIDHI MCHANGO WA SH. MILIONI 2.3 KUONDOA KERO YA UKOSEFU WA MAJI BOKO MNEMELA, PWANI

 

Na Scolastica Msewa, Boko Mnemela
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Hamoud Jumaa ameongoza Harambee ya kuchangisha shilingi zaidi ya milioni 5 ya uchimbaji wa mfereji ya kupitisha Bomba la maji la urefu wa kilo mita 1.2 ilikumaliza kero ya maji ya katika Kata ya Boko yenye vijiji vinne.

Harambee hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Boko Mnemela na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali kwa lengo la kumaliza kabisa tatizo la ukosefu wa maji ambalo kinamama utembea umbali mrefu kufuata maji.

Amesema suala la kutatua kero ya maji na ukosefu wa maji ni jambo la serikali lakini wanaoumia ni Wananchi ambapo yeye Mnec Jumaa anawaonea huruma Wananchi hivyo baada ya Uongozi wa CCM wilaya kumuomba awe Mgeni rasmi na baada ya kuona Wananchi wameshakaa zaidi ya mwaka Sasa bila maji ya Bomba ndio maana ameamua kuongoza harambee hiyo.

Alisema "kila mtu achangie kile alicho nacho ilikufanikisha uchimbaji wa mtalo huo mabomba ya maji yafikishwe hadi Boko Mnemela kero ya maji iishe".

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibaha vijijini Mkali Kanusu alisema maamuzi ya CCM Wilaya kuingilia Kati na kutafutia ufimbuzi kero hiyo ya maji ni baada ya Kamati ya siasa Wilaya kufika kijijini hapo tarehe 31 mwezi uliopita na kufanya Mkutano wa hadhara ambapo kwenye Mkutano huo robo tatu ya kero zilizoibuliwa ni kero hiyo iliyochukua sehemu kubwa ya majadiliano ilikuwa ni malalamiko ya Wananchi kukosa maji zaidi ya mwaka mmoja Sasa.

Alisema tayari CCM wilaya imekwishafanya mazungimzo na DAWASA na Mamlaka ya Usambazaji wa Maji vijijini RUWASA na wamebaini kuwa chanzo cha maji cha mpiji kimezidia kwa kuwa Bomba lililolazwa awali lilikuwa ni la saizi ya inchi 3 ambalo ni Dogo halitoshi ukilinganisha na idadi ya watu wa kuanzia temboni, Boko Timiza, ambapo pia kuna viwanda vimepelekewa maji.

"Sasa Bomba ni Dogo ambalo limeungwa na wengi wenye matumizi makubwa kule mwanzo kwa hiyo matumizi ya maji kule ni makubwa yanafanya maji huku Boko Mnemela yasifike kwahiyo nilizungimza na injinia baada ya kile kikao akasema kwasasa hakuna la kufanya katika kutekeleza huo mradi maana hatuna fungu la kutekeleza huo mradi kwa kuweka mabomba makubwa yatakayosambaza maji kuanzia Temboni hadi huku"

"Tukakubaliana sisi kama Chama tuzungumze na wanachama wetu na Wananchi wetu kuongeza kuchimba mtalo huo wa kilo mita moja na point mbili na wenzetu wachimbe kilomita 1.8 ili kutimiza kilomita tatu ili Bomba kubwa lilazwe na maji yafike huku kwa urahisi" alisema.

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Kibaha vijijini Bernard Ghaty alisema harambee hiyo ni kutekeleza sera ya CCM kwa vitendo na sio kwa maneno Tena maana CCM ya Sasa ni ya vitendo sio ya maneno matupu.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Boko Mohamed Chawawa alisema tatizo la kukosekana ka maji ni la muda mrefu hata aliwahi kufika Mbunge wa jimbo hilo Mwakamo aliyefika kijijini hapo kuzungumza na Wananchi hawakupata suruhisho la kero hiyo zaidi ya kuonekana kwamba Wananchi walikataa kuchimba mtalo huo lakini sisi CCM kata ya Boko Mnemela tukaona Haiwezekani sisi ndio tunaopata shida na wamama wao ndio wanapata shida huku juhudi mbalimbali zilifanyika bila ufimbuzi.

"Ndipo tukaona tutafute Mtu wa kutusaidia tukaandika barua CCM mkoa ilitumpate Mnec wetu aje kuongoza hii harambee na kuja kwake ni kuthamini kilio cha muda mrefu cha Wanaboko viongozi wanaumia wakiona bado Wananchi wanaumia wakati Rais Dr  Samia anaagizo la kumtua mama ndoo kichwani" alisema.

Diwani wa Kata ya Boko Mnemela Paulo Bonface alisema zaidi ya mwaka sasa kwa upande wa serikali pamoja na jitihada zao lakini hazikutoa jawabu la kumaliza kero ya maji katika Kata hiyo wamekuwa wakipata majibu tu lakini kero iliendelea kubaki pale pale.

'Ndipo nikasema ni Bora tu Sasa Chama kiingilie Kati ilikushighulikia suala la maji, nanikushukuru sana Mwenyekiti kwa wepesi wako na Leo harambee imefanya fedha zimepatikana mfereji utachimbwa ili maji yafike Boko maana tunahitaji kunywa maii na sio vinginevyo" 
+++++++++
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa kushoto, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha vijijini Mkali Kanusu sh. milioni 2.3 alizochangia kwa niaba ya Wana CCM Kata ya Boko kwa ajili ya kuchimba mtaro wa Bomba la maji kutoka Tumbi hadi kijiji cha Boko Mnemela kumaliza kero ya ukosefu wa maji. (Na Scolastica Msewa)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages