LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 21, 2023

DC KASILDA ATEMBELEA SHULE ILIYOEZULIWA PAA KWA UPEPO

 Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni leo  ametembelea na kukagua  Majengo ya shule ya  Msingi Kalemane ambayo baadhi ya paa zake za madarasa  zimepeperushwa na upepo Mkali pia na kushuhudia  usalama Mdogo wa wanafunzi ambao wanasoma katika Shule hiyo 


Baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kalemane  iliyopo kata ya  Maore wilaya ya Same, Dc Kaslida amewapongeza wananchi kwa kuonesha  juhudi kubwa wanazozifanya hili kuchangia majengo hayo kujegwa kwa haraka. 

Akizungumza na viongozi wa shule hiyo na kuwatoa wasiwasi kuwa serikali ipo bega kwa bega  pamoja na  wananchi wao waliojitokeza katika  kushirikiana kwa pamoja kwa  kuchangia  ujenzi wa madarasa hayo na ameiagiza  Ofisi ya  Halmashauri ya wilaya hiyo kushirikiana na wananchi lengo wanafunzi waweze kupata Madarasa bora na kusoma bila ya Matatizo yoyote 

DC Kaslida ametoa maagizo kwa Ofisi ya Almashauri ya Same pia kubomoa Majengo hayo haraka hiwezekavyo ambayo yametokana  na kupata nyufa  kwa ndani na nje kwenye hizi Mvua zinazoendelea kunyesha hili kukarabatiwa Upya na kuepusha usumbufu wanaopata baadhi ya wanafunzi kwenda kusoma shule ya jirani.

Mbali na hayo yote DC Kaslida amemshukuru Afisa Elimu kata ya Maore kihoko Stephen pamoja na wananchi kwa ujumla wao kwa kuonesha ushirikiano wa kuweza kutoa hamasa ya michango wa ujenzi wa madarasa hayo na kuwahaidi kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais  wetu Samiha Suluhu Hassani  itashirikiana nao kwa pamoja hili majengo hayo yaweze kujegwa kwa haraka zaidi






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages