Eneo hili la kituo cha Daladala Machinga linatarajia kuhudumia takriban idadi ya Daladala zaidi ya 850 ambazo zitakuwa zikipita katika mizunguko ya mbalimbali.
LATRA imeandaa utaratibu wa njia ambao Daladala zote zitafika hapo zikipita katika mizunguko iliyoandaliwa kama ifuatavyo:-
Daladala Zote zitakazotoka Maeneo ya Ihumwa, Nanenane,
Swawa, Udom na Benjamin Mkapa hospital zitapita
mzunguko wa Bohari, kuja Mzunguko wa uelekeo wa hospital
ya Mkoa, zitakuja mpaka eneo la Majengo kupita
Mshikamano, zitakuja mpaka mzunguko wa Barabara ya bahi
na kuingia hapa kituoni.
Kisha zikishapakia abiria zitaondoka
hapo kupitia mzunguko wa uwanja wa ndege, zitapita eneo la
chako ni chako, zitapita Nyerere square kuja mzunguko wa
hospitali ya mkoa zinakata kushoto uelekeo wa barabara ya
Morogoro na kuendelea na safari zake.
Daladala zitokazo eneo la Veyula, Msalato, St Gema na
Chang’ombe Juu zitakuja moja kwa moja mpaka mzunguko
wa barabara ya Bahi na kuingia kituoni hapa kisha
zitaendelea kupitia mzunguko wa uwanja wa ndege kupita
Chako ni Chako, Nyerere square, Mzunguko wa Hospital ya
Mkoa, Majengo sokoni, Mshikamano, Mzunguko wa Barabara
ya Bahi zitaingia hapa Machinga kuendelea kupakia abiria
kisha zitatoka na kuelekea uelekeo wa safari zake.
Pia Daladala zitokazo Nala, Mnada mpya na Nkuhungu
zitakuja moja kwa moja kuingia hapo kituoni, zitapita kuelekea
Mzunguko wa Uwanja wa Ndege, kuelekea Chako ni Chako,
Nyerere square, Mzunguko wa Hospital ya Mkoa, Majengo
sokoni, Mshikamano, Mzunguko wa Barabara ya Bahi
zitaingia hapo Machinga kuendelea kupakia abiria kisha
zitatoka na kuelekea uelekeo wa safari zake.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇