LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 26, 2023

WAZIRI AWESO ASHIRIKI KIKAO UN KUJADILI FURSA ZA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MAJI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa tatu kushoto) akiwa katika  Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameshiriki kikao cha umoja wa Mataifa cha kujadili Uboreshaji wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira.


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameshiriki kikao cha umoja wa Mataifa cha kujadili Uboreshaji wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira kinachoratibiwa na Serikali ya Uholanzi kwa kushirikiana na UNICEF, SWA na IRCWASH chini ya uenyekiti wa Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander ambaye ameongoza kikao hicho.


Kikao hicho kilichohudhuriwa na Uholanzi na wadau hao  kimebeba ajenda ya usafi wa mazingira ikiwemo kujadili maswala mbalimbali hasa juu ya fursa ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya maswala ya Maji na usafi wa mazingira (sanitation).


Kikao hicho cha Wakuu wa Nchi wa Serikali pamoja na mawaziri wa Maji ni sehemu ya ratiba ya mikutano midogo ya Maji ya Umoia wa Mataifa New York Marekani.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages