Moja ya kiongozi wa dini Askofu wa Jimbo la Kagera Bishop Pius Byamungu
Na Lydia Lugakila, Kyerwa
Viongozi wa dini Wilayani Kyerwa wameipongeza Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa namna ilivyopiga Hatua katika Maendeleo hata katika ukusanyaji wa mapato jambo lililopelekea Halmashauri nyingine kwenda kujifunza ufanisi wa ukusanyaji mapato Wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Viongozi wa dini Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera katika kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika Wilayani humo.
Akizungumzia hatua hiyo Askofu wa Jimbo la Kagera Pius Byamungu na Padre Alex Ssenfuma wamesema licha ya Wilaya ya Kyerwa kuwa Mpya na Changa lakini bado wamezidi kupaa katika mfumo wa ukusanyaji mapato.
"Nawapongeza Viongozi wa Wilaya hii Mwenyekiti wa Halmashauri Mkurugenzi mtendaji, Katibu Tawala na Madiwani hakika kazi mmeifanya ni juzi tu tumewashuhudia Viongozi wa Wilaya jirani wakija hapa kupata somo la ukusanyaji mapato hongera sana" alisema Bishop Pius.
Aidha Viongozi hao wametumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi Wilayani humo kujikita zaidi katika masuala ya uzalishaji na kuwa walinzi katika maeneo yao kwa kutoruhusu miradi ya Serikali kuharibiwa.
Aidha wameipongeza Rais Dkt Samia kwa namna alivyoipendelea Halmashauri hiyo katika Miradi mbali mbali ya Maendeleo ikiwemo Barabara za vijijini kupitika bila usumbufu.
Katika hatua nyingine Viongozi hao wameweka msimamo wao katika Kupambana na Mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kuendelea kulaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoonekana mtandaoni.
"Katika hili tumejipanga hatutaki taifa letu kutiwa doa katika Nyumba zetu za ibada tutalipigia kelele mara moja" alisema Shekhe wa Wilaya ya Kyerwa Nuhu Badiru.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇