Mar 16, 2023

UVCCM DODOMA WAFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA+video



Katika kuadhimisha miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita, Dkt Samia Suluhu Hassan, Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dodoma leo Machi 16, 2023, wametembelea miradi mbalimbali ya mkakati ukiwemo Mradi wa Mji wa Serikali Mtumba na kupata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi huo kutoka kwa Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe.

Wajumbe hao walioongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, wametembelea miradi mingine ya ujenzi wa Reli ya Mwendokasi SGR, Shule ya mfano ya Iyumbu, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato na ujenzi wa barabare pete.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba akijadiliana jambo na Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe.
Baadhi ya majengo ya wizara  na taasisi za serikali yakiendelea kujengwa katika mji huo wa kiserikali.

Barabara za mji huo zikiwa zimejengwa

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Bandawe akieleza mafanikio ya ujenzi wa Mji huo wa serikali huku viongozi wa UVCCM Dodoma wakitoa shukrani zao...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages