MSAFARA wa kwanza wa Simba ulioondoka leo jioni Dar es Salaam kwenda Morocco kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Raja Casablanca Aprili 1 umelazimika kuishia Arusha.
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema hiyo imetokana na ndege waliyokuwa wanasafiria kupata hitilafu baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni ya leo.
Sasa msafara huo utaunganisha safari mapema kesho asubuhi kwenda Morocco.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇